Imani Potofu Kuhusu Jehanamu

Katika lugha ya Kiingereza, kwa watu wengi, neno “kuzimu” (“hell”) hutumika kama neno bayawakati watu wana hasira. Kwa wengine, neno “kuzimu” huleta mawazo yanayotisha kuhusu mateso ya milele kuungua katika shimo kwa wanadamu ambao waliisikia kanisani au kutoka kwa mwinjilisti. Haitegemei upo ndani ya jamii gani ya watu, inaonekana, kana kwamba wengi, kama si sisi sote tunafikiri ingekuwa bora ikiwa dhana ya kuzimu tu haikuwepo kabisa. Kwa kweli, baadhi, katika kujaribu kuondoa wazo hili la kutisha akilini mwao, hufanya uchaguzi wa kutokuamini katika wazo la kuzimu kabisa, na hii mara nyingi hupelekea hatua ya pili ya kuchagua kutokuamini katika Mungu ambaye angeweza kuumba kitu kama hicho.

Hivyo tunafanya nini na wazo hili la kutisha la kuzimu? Je, tulitupilie mbali wazo hili pamoja na Mungu pia? Je, tujaribu kulipuuzia na kile linachomaanisha kuhusu Mungu ni nani? Je, tunadhani kuwa walimu wetu wa Shule ya Jumapili walifanya makosa? Katika kijarida hiki cha Biblia tutachagua njia nyingine rahisi ambayo ni kujifunza tu kile Biblia isemacho kuhusu jehanamu, na kwa kufanya hivyo utagundua kwamba ukweli utakuweka huru dhidi ya imani mbalimbali potofu kuhusu fundisho hili la kutisha.

Linalovutia ni kuwa, Biblia inatupatia maelezo kamili kuhusu lini jehanamu itaanza na mahali inakopatikana. Kama unavyofahamu, kuna mawazo mengi ya uongo kuhusiana na mambo haya mawili. Yesu anazungumza wazi katika Mathayo 13:49, “Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia: malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” Kulingana na fungu hili na mengineyo mengi: (1) Miale ya moto wa jehanamu haitawaka hadi dunia itakapofika mwisho. Hiyo ni sahihi! Wapendwa wako hawachomwi moto wakiwa hai unapokuwa ukisoma kijarida hiki.
Pia, tunaona kwamba Mtume Petro hutupatia maelezo kamili kuhusu mahali jehanamu itakapokuwa. Akizungumzia kuhusu mwisho wa dunia anasema, “Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.” (2) Nabii Sefania pia huizungumzia hivi, “Dunia yote,” itaangamizwa “itateketezwa kwa moto wa hasira ya Mungu.” (3) Hapa tunaona kuwa jehanamu sio shimo kubwa katikati ya dunia; badala yake; itakuwa hapa hapa duniani wakati wa mwisho wa dunia ikiiteketeza “nchi yote.”

Huenda kitu muhimu tunachopaswa kuelewa kuhusu kuzimu kinaweza kupatikana katika fungu maarufu la Yohana 3:16, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.” Hapa Yesu anaweka bayana kwamba ni wale wanaomwamini ndio ambao huishi milele, sio waovu. Nini? Waovu hawaishi milele wakiungua moto? Umesoma sawa sawa! Hawaungui milele!

Waovu wanapaswa kuungua mpaka kusiwepo na kitu chochote kinachobaki kuungua. Malaki huelezea jambo hili vyema: “Kwani tazama siku inakuja, iwakayo kama tanuru, na wote wenye kiburi, naam na wote watendao uovu watateketezwa kama vile makapi. Na siku hiyo inayokuja, itawateketeza wote,” (4) Kwa kweli, hivi tunaweza kuwa na uhakika kwamba alikuwa akiongea kwa uhalisia kuhusu kuangamizwa kabisa kwa waovu, anaendelea kusema, “Nanyi mtawakanyaga waovu, kwani watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu siku ile nilifanyapo hili asema Bwana wa majeshi.” (5) Pia, siyo tu kwamba waovu watateketezwa kabisa katika moto wa jehanamu lakini pia Shetani pamoja na malaika zake waovu kulingana na Mt. 25:41 na Ufu. 20:10. Kinyume na imani iliyoenea, Mungu anapanga kuziangamiza nguvu za giza, na siyo kuziweka kusimamia shimo la moto wa milele katika kitovu cha dunia!

Lakini wengine wanaweza kusema kwamba kuna mafungu mengine kama vile Ufunuo 14:11 na Ufunuo 20:10 ambayo huelezea kuwa waovu watateketea milele. Vema, Biblia pia inasema kuwa nabii Samweli angeendelea kukaa hekaluni mwa Bwana milele, (5) na kwamba kamba za dunia zilimfunga Yona milele (6) alipotupwa baharini. Sasa ni dhahiri kutoka katika Maandiko kuwa kati ya matukio haya hakuna tukio lililodumu milele. Tunachokiona hapa ni jinsi Biblia inavyoitumia lugha ya mfano ya neno “milele” kumaanisha muda usio na ukomo wa jambo ambapo mwanzo na mwisho wa kipindi hicho hutegemea asili ya mtu fulani, mazingira, au vitu vinavyotumika. Mfano halisi wa wakati wetu ambao unaofanana na maelezo hayo ni wakati mume na mke wanapoapa kuishi katika ndoa yao milele. Wanapokuwa wakifanya hivyo, neno “milele” humaanisha “kulingana na muda watakaoishi”. Hivyo je, tunajuaje “milele” ya waovu itakuwa ni muda gani? Ni rahisi. Mafungu mengine huelezea kwamba “milele” katika muktadha huu humaanisha mpaka pale waovu wanapoteketezwa kabisa.

Kutokana na nuru tuliyoipata katika mafungu haya rahisi ya Biblia, mtu mmoja huenda akauliza, “Je, inakuwaje basi imani hizi potofu kuhusu jehanamu zinaendelea kuwepo?” Ukweli ni kwamba mafundisho haya ya uongo miongoni mwa madhehebu mengi ya Kikristo sio tu mbinu nzuri inayotumika kuogopesha watu ili wahudhurie kanisani, lakini ni kwa sababu mshitaki wetu, ibilisi hupenda kufundisha uongo kuhusu Mungu. Katika kitabu cha Ufunuo 12:9 Shetani ameelezewa kama mmoja “audanganyaye ulimwengu wote.” Huwadanganya watu kuhusu nini? Kuhusu ukweli wa Mungu na tabia yake. Ndiyo, kuna mafundisho ya kweli na ya uongo kuhusu Mungu katika ulimwengu huu. Ukweli sio uchaguzi, kama ambavyo wengi wangependa kuamini hivyo. Ukweli ni uhalisia unaosubiri kugunduliwa katika kurasa za Maandiko Matakatifu. Na uhalisia ni kuwa, ndiyo, “Mungu wetu ni moto ulao,” (7) kwa dhambi na wadhambi. Lakini Biblia hufundisha kuwa, mbali na waovu, ni watakatifu, “waendao kwa ukamilifu na kutenda haki,” ndio ambao “watakaa na kuishi mbele ya moto uteketezao” na “kuunguza milele.”(8)

Ni kweli! Kulingana na Mathayo 25:31-46, wanadamu wote siku moja watakutana na Mungu ambaye mbele zake “milima huyeyuka, na dunia huteketea,(9) bali ni wale tu ambao wameziungama dhambi zao na kumtafuta Mungu ndio watakaoweza kulindwa mbele zake ndani ya moto ambapo wataishi milele zote. Kwa upande mwingine, waovu “hawatakuwepo” na “itakuwa kana kwamba hawajawahi kuishi,” (10) baada ya kuwa “wameangamizwa na uharibifu wa milele kutoka mbele za Bwana na kutoka katika utukufu wa uweza wake.” (11) Marafiki, “Mungu ni pendo,”(12) upendo ambao huwakilishwa na alama ya moto. Sulemani alisema upendo wa Mungu . . . unao mn’gao kali.”(13) Kama vile moto uufanyavyo udongo wa mfinyanzi kuwa mgumu, lakini huyeyusha barafu, hivyo ndivyo upendo wake utakavyomfariji mtakatifu lakini utamwangamiza mwenye dhambi. Leo, unao uchaguzi, kuufanya moyo wako mgumu kwa Mungu au kuiruhusu miale yake ya moto ikuyeyushe. Uchaguzi wowote ule tuufanyao huamua jinsi umilele wetu utakavyokua, lakini Mungu hubaki kuwa yule yule. Mtafute leo, na upendo wake utakuwa moyoni mwako milele zote!

Mifano:
1) Mathayo 25:31-41; 2 Pet. 3:3-7, 12
2) 2 Petro 3:10
3) Sefania 1:18
4) Malaki 4:1, 3
5) 1 Samweli 1:22
6) Yona 2:6
7) Waebrania 12:29
8) Isaya 33:14, 15
9) Nahumu 1:5
10) Obadia 1:16
11) 2 Wathesalonike 1:9
12) 1 Yohana 4:8
13) Wimbo Ulio Bora 8:6